Kiungo mpya wa majogoo wa Anfield Liverpool Naby Keita amefunguka na kusema kuwa alitamani sana kucheza kama kiungo wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard enzi za utoto wake wakati akicheza mpira mtaani nchini kwao Guinea.
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani kwa uhamisho wa ada ya Euro mil 57,tayari amekabidhiwa jezi yeye namba 8 mgongoni ambayo alikuwa akiivaa mkongwe huyo ambaye kwa sasa ni kocha katika klabu ya Rangers.
akiongea na kituo cha Espn Keita amesema “Baba yangu alizungumza na mimi nilipojiunga na Liverpool na amenieleza jinsi gani anavyoipenda Liverpool hata sisi wakati tunacheza mpira mtaani tulikuwa tukivaa Jezi za Liverpool.”

